Makubwa! Willy Paul na wenzake waambiwa Injili sio uwanja wa kusakia umaarufu

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Reuben Kigame, amewafichulia siri waimbaji chipukizi wa Injili Kigame anawasisitizia nia ya kuandika miziki kuhusu neno la Mungu na kulizingatia kwa moyo na nafsi

– Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Reuben Kigame, amewafichulia siri waimbaji chipukizi wa Injili

– Kigame anawasisitizia nia ya kuandika miziki kuhusu neno la Mungu na kulizingatia kwa moyo na nafsi

– Anawataka vijana katika muziki wa Injili kuimba na kutenda na wala sio tu kupitisha ujumbe

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Reuben Kigame, amewafichulia siri waimbaji chipukizi wa Injili na kuwaeleza namna ya kuhakikisha wanafaulu.

Habari Nyingine: Kuingia Mombasa rahisi, kutoka matanga-hii ndiyo sababu

Kigame anawasisitizia vijana nia ya kuandika miziki kuhusu neno la Mungu, na kulizingatia kwa moyo na nafsi kila wanapoimba.

“Ukiandika wimbo kuhusu neno la Mungu, nukuu, litumie, nakuahidi, wimbo wako utakuwa mkubwa zaidi yako. Utakuwa mkubwa kama Neno la Mungu na hautakuwa rahisi kutoweka masikioni mwa watu,” Kigame ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook ujumbe ambao TUKO.co.ke imeusoma.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Limousine ya KSh208 M iliyo na uwezo wa kwenda ardhini na majini (Picha)

Kwa muda sasa, kumekuwapo na maoni kwamba, wasanii wengi Kenya wa muziki wa Injili hawana mvuto, na wengi wao huwa hawadumu.

Kigame anawataka vijana katika muziki wa Injili, kuimba na kutenda na wala sio tu kupitisha ujumbe bila ya kufanya kwa matendo.

Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!

Habari Nyingine:Je wanaume wanahitaji nini katika uhusiano? Wakenya watoa maoni yao Kagame anawasihi wasanii kuandika na kuimba muziki unaoeneza Injili kikamilifu, na kuacha kuimba mambo ambayo wenyewe hawayazingatii.

“Badala ya kulalamika muziki wa siku hizi hauna mafunzo, tafadhalini watu wa Mungu, fundisheni Neno kwa uaminifu na litapenya kupitia nyimbo mlizoandika na kubadilisha maisha kwa kuwa Mungu hulitii Neno lake Mwenyewe,” Kigame ameshauri.

Habari Nyingine:Pasta ahamishwa kwa nguvu Baba Dogo kwa kuwakataza waumini kula nyama!

Kigame anaamini ushauri wake utachangia zaidi katika kuboresha utunzi wa muziki wa Injili na kusaidia kubadilisha maisha.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4B3fI9mpJqjpZfEonnWoqOlsV2lrra4jKeYZq%2BVo8eit8RmrpqZnZe2uK2MoqWjoZyeerS1zmassJmen65uw8Bmoq6rkaC2onnUppiaqqWbwm%2B006aj

 Share!